Swahili: Mwenendo Wa Kufuata

Uchunguzi uliofanywa na Child Soldiers International, maagizo ya Kamati ya Haki za Mtoto kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na mashauri ya makundi yasiyokuwa ya serkali ya humu Congo, yamesaidia Child Soldiers International kutunga mradi ambao ukomo wake ni kufanya mkaguo wa mipango ya kupokonya silaha na kuishi vizuri katika jamii (DDR) kwa ajili ya vijana wanawake wa chini ya myaka 18 wenyi kuwa katika makundi yenyi kumiliki silaha mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Katika mradi huo, kundi moja la uchunguzi limepitisha juma sita katika majimbo ya Kivu ya Kusini, Kivu ya Kaskazini na Uele ya Juu mwanzo wa mwaka wa 2016. Kundi hilo limezungumza na vijana wanawake 150 waliokuwa zamani katika makundi ya wanaomiliki silaha1 , wanamemba 84 wa mtandao wa jamii kwa kukinga mtoto (Réseaux communautaires de protection de l’enfant: RECOPE), waalimu na waongozi wa masomo 12, waongozi wa makanisa 8, wanaousika na watumishi 46 wanaousika na mipango ya DDR na wajumbe 14 wa wakubwa wa miji. Ukomo wa mazungumzo hayo ulikuwa kujua namna gani vijana wanawake wanasaidiwa na mipango ya DDR, na kuangalia kama ma kazi hayo yote - hapo yanapofanyika - yanapatana, hasa zaidi kulingana na vijana wanawake wenyewe.

Majifunzo yaliyopita yameonyesha waziwazi2 kama miongoni mwa watoto waliotoka katika makundi ya-nayomiliki silaha, hesabu ya vijana wanawake ni ndogo, hawapati msaada wa DDR sawa na vijana wanaume, na, ikiwa wameupata, haupatani na mahitaji yao ya kipekee. Kwa namna ya pekee, majifunzo yemeonyesha kwamba, ijapo matendo mbalimbali kwa ajili yao, vijana wanawake wanabaguliwa na kusemwa vibaya wanaporudi katika jamii. 

Tena, mipango ya DDR haileti jibu la kutosha kwa magumu hayo wanaopata kwa kupokelewa katika jamaa na katika jamii.

Mwezi wa kumi, mwaka wa 2016, Child Soldiers International ameleta ripoti ya uchunguzi wake katika mku-tano wa pale Goma mbele ya wanamemba wa DDR, Ofisi mbalimbali ya Umoja wa mataifa, makundi ya-siyokuwa ya serkali (ONG) na wajumbe wa serkali. Waliohuzuria mkutano huo, wamesikiliza malalamiko na maagizo ya vijana wanawake yaliyoletwa na Child Soldiers International. Pia walifikiria kuhusu majibu kwa hayo yote kabla ya kukusudia nini itafinyika kwa ajili ya mahitaji ya vijana wanawake na kurahisisha, katika heshima ya haki zao, kwa kupokonya silaha na kwa kurudia katika maisha ya jamii.

Kitabu hiki ni mchango wa mawazo yaliyoletwa katika mkutano wa Goma. Ni kama « sanduku ya vyombo » kwa kuwasaidia wanamemba wa DDR ili kuwashurulikia vijana wanawake waliokuwa katika makundi ya-nayomiliki silaha mashariki mwa Congo, katika mahitaji yao. « Sanduku ya vyombo » hii itawasaidia vilevile wanamemba hao kupiganisha na kushinda vikwazo ambavyo vijana wanawake wanavipata, ginsi walivyo-sema wao wenyewe3, katika mpango wa kupokonya silaha na kurudia katika maisha ya kijamii. Mawazo mengi ya kitabu hiki si mapya. Makundi mengi yasiyokuwa ya serkali (ONG) yamekwisha kuyatumia mara nyingi. Lakini, mawazo hayo hayajulikani sana wala hayatumiwi vema na wanamemba wote wa DDR.

Soma kitabu hapa.

Pia inapatikana ndani: Kiingereza, Kifaransa, Lingala